KASULU IMESIMAMA

Hao ni baadhi ya mashabiki wa soka wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakifuatilia kandanda katika uwanja wa Umoja Kasulu linakopigwa soka la MON FM SUPER CUP 2025

Michuano hiyo ambayo imeratibiwa na kusimamiwa na Mon FM Radio imeanza July 25, 2025 kwa kuzinduliwa na mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isac Mwakisu inashirikisha timu 12 kutoka mjini Kasulu ambapo inatarajia kufanyika kwa muda wa mwezi mmoja.

Wadhamini mbalimbali wamejitokeza kudhamini michuano hiyo ambayo imepokewa kwa shangwe kubwa mjini Kasulu.

miongoni mwa wadhamini waliojitokeza kudhamini michuano hiyo ni pamoja na:- Nyarubanda Phamacy, Kilima digital printing , Mpema Media, TAKUKURU Kasulu, Mwiza Min Super Market, Vitolian Health Center, Serengeti night Park, DAKAMU Investment, CRDB Bank na YAS

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *